
WENYEJI
Gabon wametupwa nje ya AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika, baada ya kutoka Sare 0-0 na Cameroon huko
Libreville katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi A.
Sasa
Cameroon na Burkina Faso, ambao Jana waliifunga Guinea-Bissau 2-0,
wamesonga Robo Fainali huku Burkinabe wakiwa Washindi wa Kwanza wa Kundi
na Cameroon ni wa Pili.
Nchi nyingine ambazo zimetinga Robo Fainali wakiwa na Mechi 1 mkononi ni Senegal na Ghana.
Leo zipo Mechi za mwisho za Kundi B ambapo Senegal watacheza na Algeria na Zimbabwe kuivaa Tunisia huku Algeria na Tunisia zikisaka kuungana na Senegal Robo Fainali na Zimbabwe ikikamilisha Ratiba tu.
0 Maoni:
Post a Comment