REAL MADRID WASOGELEWA KWA UKARIBU ZAIDI.

 Tokeo la picha la LA LIGA IMAGE
JANA Timu ambazo zinawakimbiza Vinara Real Madrid, Sevilla na Barcelona, zote zimeshinda na kuleta presha kwa Real ambao wamecheza Mechi 1 pungufu.
 
Wakati Real wamecheza Mechi 18 na wana Pointi 43, Sevilla wanafuatia wakiwa na Pointi 42 kwa Mechi 19 na Barca wamecheza Mechi 19 na wana Pointi 41.
 
Timu ya 4 ni Atletico Madrid wenye Pointi 35 kwa Mechi 19.
Hapo Jana, Barca wakicheza Ugenini waliitandika SD Eibar 4-0 kwa Bao za Denis Suárez (Dakika ya 31'), Messi (50'), Luis Suárez (68' ), na Neymar (90'+1).
 
Katika Mechi hiyo Barca walipata pigo mapema baada ya Kiungo wao wa kutegemewa Sergio Busquets kuumia na Denis Suarez kuingizwa na kuwapatia Bao la kwanza kwa Mkwaju wa Mita 20.
 
Nayo Timu ya Pili Sevilla ilipigana na hatimae kuishinda Ugenini 4-3 Osasuna.
 
Osasuna walifunga Bao zao Dakika za 15, 63 na 90.kupitia Sergio Leon, Fuente, aliejifunga mwenywe, na Kenan Kodro.
Bao za Sevilla zilipachikwa na Fuente Dakika za 43 na 65, na nyingine ni Dakika za 80 na 90 kupitia Franco Vazquez na Pablo Sirabia.
 
Atletico Madrid walitoka 2-2 Ugenini na Athletic Bilbao waliofunga Bao zao kupitia Inigo Lekne na Oscar De Macos Dakika za 42 na 56 wakati za Atletico zikipigwa na Koke na Antoine Griezmann kwenye Dakika za 3 na 80.
 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment