
MAHASIMU
wa Jadi huko England, Manchester United na Liverpool wametoka Sare 1-1
katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Uwanjani Old Trafford
Mjini Manchester.
Kwenye
Mechi ya Kwanza ya EPL Msimu huu Timu hizi zilitoka 0-0 huko Anfield na
Leo Man United waliingia kwenye mtanange huu wakiwa hawajafungwa katika
Mechi 15 zilizopita huku wakishinda Mechi 6 za EPL mfululizo wakati
Liverpool, baada ya kuichapa Man City 1-0 Desemba 31, hawajashinda hata
Mechi baada kufungwa 1 na Sare 2.
Lakini jana Liverpool walianza vyema kwa kufunga Bao la Penati ya Dakika ya 27
iliyopigwa na James Milner ambayo ilitolewa baada ya Kona ya Milner
kudaiwa na Refa Michael Oliver ilishikwa kwa makusudi na Paul Pogba
wakati Kiungo huyo wa Man United hakuwa akitazama Mpira na wala hakuinua
Mkono juu akiwa kwenye harakati za kummaki Mchezaji wa Liverpool Dejan
Lovren, kitu ambacho Wachambuzi wengi huko England walikiunga mkono.

Licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga, Man United walingojea hadi Dakika ya 84 pale Zlatan Ibrahimovic aliposawazisha
baada kutokea kizaazaa langoni mwa Liverpool kufuatia Kichwa cha
Marouane Fellaini kugonga Posti na kumrejea Ibrahimovic aliefunga.

JE WAJUA KUHUSU HII?
- Zlatan Ibrahimovic amefunga Bao 14 katika Mechi zake za kwanza 20 za EPL akifungana na Lejendari Alan Shearer na Sergio Aguero.
Matokeo
haya yamewaweka Liverpool Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 45 sawa na Timu
ya Pili Tottenham huku Vinara Chelsea wakiongoza wakiwa na Pointi 52.
Man
United wako pale pale Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 40 na Nafasi ya 5
wako Man City wenye 42 na Arsenal ni wa 4 wakiwa na Pointi 44.
Mechi
zijazo kwa Timu Man United na Liverpool ni Jumamosi ijayo wakati
Liverpool wako kwao Anfield kucheza na Swansea City wakati Man United
wako Ugenini kuivaa Stoke City.
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED: De
Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian [Fellaini 76'], Carrick [Rooney
45'], Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial [Mata 65'] Ibrahimovic
Akiba: Romero, Fellaini, Blind, Smalling, Rooney, Mata, Rashford
LIVERPOOL: Mignolet, Alexander-Arnold, Lovren, Klavan, Milner, Henderson, Can, Lallana, Wijnaldum, Firmino, Origi [Coutinho 61']
Akiba: Karius, Gomez, Moreno, Stewart, Ejaria, Coutinho, Sturridge
![]() |
Michael Oliver |
0 Maoni:
Post a Comment