
EVERTON jana huko Goodison Park imewaonyesha Manchester City kwamba wao wapo juu kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, kwa kuwatandika Bao 4-0 kipigo ambacho ni kibaya mno kwa Meneja wa City katika himaya yake kwenye Mechi za Ligi.
City walikuwa nyuma 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Romelu Lukaku la Dakika ya 34.

Kipindi
cha Pili Everton wakatandika Bao nyingine 3 katika Dakika 47, 79 na 90
Wafungaji wakiwa Kevin Mirallas na Chipukizi Tom Davies na Ademola
Lookman.

Matokeo hayo yamewaacha City wakiwa Nafasi ya 5 na Everton wakiwa Nafasi ya 7.
Mechi
inayofuata kwa City ni Jumamosi ijayo wakiwa kwao Etihad kucheza na
Timu ngumu Tottenham Hotspur wakati Everton wako Ugenini huko Selhurst
Park kucheza na Crystal Palace.
VIKOSI VILIVYOANZA:
EVERTON: Robles, Holgate, Ashley Williams, Funes Mori, Coleman, Davies, Barry, Baines, Barkley, Mirallas, Lukaku
Akiba: Schneiderlin, Jagielka, Lennon, McCarthy, Valencia, Stekelenburg, Lookman.
MAN CITY: Bravo, Sagna, Otamendi, Stones, Clichy, Zabaleta, Touré, Silva, De Bruyne, Sterling, Agüero
Akiba: Kolarov, Caballero, Jesus Navas, Delph, Sané, Iheanacho, García.
![]() |
Mark Clattenburg. |
0 Maoni:
Post a Comment