MENEJA wa Liverpool Jürgen Klopp
amesisitiza Msimu wao haujapotea na Timu yake inaweza kufufua matumaini
ya Ubingwa kwa Leo kuwafunga Chelsea Uwanjani Anfield kwenye Mechi ya
EPL, Ligi Kuu England.
Liverpool wameporomoka hadi Nafasi ya 4 kwenye EPL wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea walio chini ya Meneja Antonio Conte.
Ndani ya Wiki moja iliyopita, Liverpool wametupwa nje ya Makombe
Mawili, EFL CUP na FA CUP, wakipokea vipigo vitatu mfululizo Nyumbani
kwao Anfield ambako hawajafungwa Mechi 4 mfululizo tangu Mwaka 1923.
Kipigo cha 4 hakitaki Klopp na safari hii anacheza na Chelsea ambayo Mwezi Septemba aliichapa huko Stamford Bridge Bao 2-1.
Baada ya kurejea kwa Sadio Mane kikosini akitokea huko Gabon kwenye
AFCON 2017 alikokuwa akiichezea Nchi yake Senegal, Klopp anaweza
kuwachezesha kwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu Novemba 6 walipoinyuka
Watford 6-1, Mastaa wake kina Sadio Mané, Philippe Coutinho, Roberto
Firmino na Adam Lallana ambao ni kombinesheni kali ya Mashambulizi.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Henderson, Can, Firmino, Coutinho, Lallana, Mane
Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Matic, Kante, Alonso, Hazard, Pedro, Costa

Mark Clattenburg
0 Maoni:
Post a Comment