BARCELONA YATUMA SALAMU REAL MADRID.

Tokeo la picha la SUAREZ IMAGE VS LAS PALMERS IMAGE

MABINGWA wa La Liga huko Spain, FC Barcelona, Jana waliifyeka Las Palmas 5-0 na kukamata Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Real Madrid.
 
Lakini Real wana Mechi 2 mkononi na Leo wana nafasi ya kuliongeza pengo la Pointi kuwa 5 wakicheza Ugenini na Sevilla ambayo Juzi ilishindwa kuibwaga Real dhaifu iliyocheza bila Wachezaji kadhaa maarufu akiwemo Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo walipoumwaga uongozi wa 3-1 na Real kurudisha na kuwa 3-3 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey.
 
Real, wakiwa pia na Timu dhaifu, waliinyuka Sevilla 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey.
Tokeo la picha la SUAREZ IMAGE VS LAS PALMERS IMAGE
 
Bao za Barca hiyo Jana zilifungwa na Luis Suarez, Bao 2, Lionel Messi, Arda Turan na Aleix Vidal.
Mapema Jana, Bao la Dakika ya 8 la Nicolas Gaitan liliipa Atletico Madrid ushindi wa 1-0 walipocheza na Real Betis.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment