FOWADI wa Arsenal Alexis Sanchez amekiri kwa Mamlaka ya Kodi huko Spain wa kukwepa Kodi ya €983 443 wakati akiichezea Barcelona.
Sanchez, Mchezaji wa Kimataifa wa Chile mwenye Miaka 28, sasa
anakabiliwa na kupigwa Faini na pengine Kifungo ambacho kinaweza kuwa
cha nje.
Akitoa ushahidi wake akiwa Jijini London, England,
Sanchez alikubali 'kosa katika stahili ya Malipo ya Kodi yake' ambayo
sasa amelipa yote.
Sanchez amekiri kuwa hesabu za Kodi yake za Miaka ya 2012 na 2013
hazikujumuisha Faida iliyotokana na Umiliki wake wa Picha na Matangazo
yake ambayo yalilipwa kupitia Kampuni yake iliyokuwa huko Malta.
Pia Sanchez alikiri kumiliki Kampuni hiyo Numidia Trading Limited ambayo hakuibanisha kwenye Malipo ya Kodi zake huko Spain.
Kesi hii inafanana na ile ya Mchezaji wa Barcelona Javier
Mascherano ambae Januari 2016 alipigwa Faini €815 000 na Kifungo cha
Mwaka Mmoja alichotumikia nje ya Gereza kwa udanganyifu wa Malipo ya
Kodi huko Spain.
Wengine waliokumbwa na kadhia kama hiyo ni Staa wa Barcelona na
Argentina Lionel Messi na Baba yake Mzazi kutwangwa Faini ya Euro
Milioni 2 hapo Julai 2016 na pia kuhukumiwa kufungwa Jela Miezi 21
Kifungo ambacho kilifanywa kiwe cha nje badala ya Gerezani.
Huko Spain Vifungo vya chini ya Miaka Miwili hutumikiwa nje ya Gereza.
0 Maoni:
Post a Comment