Mtoto wa mshambuliaji wa Uholanzi
Patrick Kluivert, Justin, mwenye umri wa miaka 17 amejitosa kwa mara ya
kwanza uwanjani akiwa na klabu ya Ajax na kupata ushindi katika mechi ya ugenini
PEC Zwolle siku ya Jumapili.
Winga Kluivert aliingia uwanjani katika dakika ya 39 baada ya Amin Younes kuumia. Mkwaju wa penalti kutoka kwa Lasse Schone uliiweka Ajax mbele na Hakim Ziyech akaongeza la pili.
Nicolai
Brock-Madsen alikomboa goli moja lakini Ziyech akaongeza jingine na
kuwahakikishia Ajax ushindi ambao unaifanya Ajax kusalia na alama tano
nyuma ya viongozi Feyenoord, iyoichapa Roda 2-0.
Babake, Kluivert
Sr, alishinda mataji mawili ya Eredivisie ya uholanzi na pia akashinda
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alipokuwa akichezea klabu ya Ajax kwa miaka
mitatu kati ya mwaka 1994 na 1997
Alienda kuichezea AC Milan,
Barcelona, Newcastle United, Valencia, PSV Eindhoven na Lille na
alifunga magoli 40 katika mechi 79 alizochezea taifa lake.
Kiungo huyo ambaye kwa hivi sasa ana umri wa miaka 40 ni mkurungezi wa mpira wa soka katika klabu ya PSG. ya Ufaransa
0 Maoni:
Post a Comment