KIUNGO
wa Arsenal Granit Xhaka amehojiwa na Polisi baada ya kuibuka tuhuma za
kumkashifu kibaguzi Mfanyakazi wa Kampuni ya Ndege Uwanjani Heathrow
Jijini London.
Xhaka,
Raia wa Uswisi mwenye Miaka 24, anaaminika kuwa alikuwa akimsindikiza
Rafiki yake aliemtembelea London na kukutwa na mkasa huo Jumatatu Usiku.
Sakata
hilo linadaiwa kutokea baada ya Mchezaji huyo wa Arsenal na Rafikiye
kuchelewa kufika Uwanja wa Ndege na Rafiki huyo kuzuiwa kupanda Ndege
kurejea Ujerumani.
Hapo
ndipo inadaiwa Xhaka alitoa maneno ya kashfa ya Kibaguzi na Polisi
wamethibitisha kutokea tukio hilo na kusema Mtuhumiwa amehojiwa na
uchunguzi unaendelea.
Klabu ya Arsenal imekataa kuzungumza lolote.
Tukio
hili la Xhaka limetokea takriban Masaa 24 tangu apewe Kadi Nyekundu
kwenye Mechi ya Ligi na Burnley ambayo Mswisi huyo alitolewa kwa Kadi
Nyekundu wakati Arsenal inashinda 2-1 kwenye Mechi ambayo
pia Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alitolewa nje ya Uwanja na Refa na
Jana kushitakiwa kwa Utovu wa Nidhamu na FA, Chama cha Soka England.
0 Maoni:
Post a Comment