Sunderland imemsaini Beki wa zamani wa England, Joleon Lescott, ambae mara ya mwisho aliichezea Aston Villa.
Lescott,
mwenye Miaka 34, aliwahi kuwa Mchezaji chini ya Meneja wa sasa wa
Sunderland David Moyes huko Everton kati ya Mwaka 2006 na 2009.
Msimu
uliopita, Lescott aliondoka Villa kujiunga na Timu ya Greece AEK Athens
na kucheza Mechi 4 tu na kuumia na Mkataba wake kuvunjwa Novemba Mwaka
Jana.
Sunderland, ambao wako mkiani mwa EPL, Ligi Kuu England, imemsaini Beki huyo kwa Mkataba mfupi wa hadi mwishoni mwa Msimu.
0 Maoni:
Post a Comment