CONGO
DR Jana waliifunga Morocco 1-0 katika Mechi ya Kundi C la AFCON 2017,
Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, kwenye Mechi
iliyochezwa huko Stade d'Oyem, Assok Ngomo Nchini Gabon.
Bao
la ushindi la Congo DR, ambao Wiki iliyopita walifanya mgomo kushinikiza
kulipwa Fedha zao, lilifungwa na Junior Kabananga katika Dakika ya 55.
Congo
DR walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 81 kufuatia Kadi Nyekundu kwa
Lomalisa Mutambala, alieingizwa kutoka Benchi, na ndani ya Dakika 16
kupewa Kadi za Njano 2.
Mapema Jana, kwenye Mechi nyingine ya Kundi C, Mabingwa Watetezi Ivory Coast walitoka 0-0 na Togo. Leo Jumanne zipo Mechi mbili za Kundi D kati ya Ghana na Uganda na kisha ni Mali na Egypt zote zikichezwa Oyem Stadium, Mjini Assok Ngomo huko Gabon.
VIKOSI VILIVYOANZA:
CONGO DR: Matampi, Nsakala, Zakuani, Tisserand, Ssama, Mulumba, Bope Mbemba, Mubele, Bakambu, Kabananga
MOROCCO: Munir, Benatia, Da Costa, Saïss, Dirar, El Ahmadi, Boussoufa, Mendyl, El Kaddouri, Bouhaddouz, Carcela
REFA: Hamada Nampiandraza [Madagascar]
0 Maoni:
Post a Comment