MABINGWA IVORY COAST YATOA SARE DHIDI YA TOGO

Picha inayohusiana
AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, yameendelea tena huko Nchini Gabon na Sare tena kutawala katika Mechi ya Kundi C kati ya Mabingwa Ivory Coast walipotoka 0-0 na Togo huko Stade de Franceville Mjini Franceville.
 
Hiyo ni Mechi ya 4 ya Fainali hizi kumalizika kwa Sare na ni Mechi 1 tu iliyotoa Mshindi hapo Jana wakati Senegal walipokuwa Nchi ya kwanza kuzoa Pointi 3 baada ya kuifunga Tunisia Bao 2-0 huko Port Gentil Stadium, Mjini Port Gentil, Nchini Gabon kwenye Mechi ya Kundi B.
 Picha inayohusiana


DONDOO ZA NDANI:

  • Mvuto wa Mechi hii ilikuwa kumwona Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, alieikana England, akiichezea Ivory Coast kwa mara ya kwanza katika Mashindano rasmi wakianza kutetea Ubingwa wao huku Togo wakiongozwa na Kepteni wao Emmanuel Adebayor ambae sasa hana Klabu tangu aondoke Crystal Palace Mwezi Juni.
  • Pia Kocha Mbelgiji Claude LeRoy, akionekana kwa mara ya 9 kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika akitwaa Ubingwa mara moja Mwaka 1988 akiwa na…., lakini safari hii akiwa na Togo ambayo haijawahi kuwa Bingwa.
  • Ivory Coast wamekuwa Mabingwa wa AFCON mara 2 kwa kuibwaga Ghana huko Senegal (1992) na Equatorial Guinea (2015) zote kwa Penati Tano Tano baada Sare za 0-0.

Baadae Jana ilikuwepo Mechi nyingine ya Kundi C kati ya Congo DR na Morocco. na Congo DR kuifunga morocco goli 1 kwa bila.

Leo Jumanne zipo Mechi mbili za Kundi D kati ya Ghana na Uganda na kisha ni Mali na Egypt zote zikichezwa Oyem Stadium, Mjini Assok Ngomo huko Gabon.

VIKOSI VILIVYOANZA:
IVORY COAST: Gbohouo, Aurier, Bailly, Kanon, Traoré, Kessié, Serey Dié, Seri, Zaha, Kodjia, Kalou
Akiba: Mande, Pepe, N'Guessan, Koné, Angban, Doukoure, Bony, Sio, Gradel, Deli, Bagayoko, Sangaré
TOGO: Agassa, Gakpe, Romao, Ouro-Akoriko, Dakonam Ortega, Dossevi, Ayité, Atakora, Bebou, Fo-Doh Laba, Adebayor
Akiba: Mensah, Atchou, Ouro-Sama, Akakpo, Mamah, Agbégniadan, Bossou, Kouloum, Boukari, Segbefia, Eninful, Tchagouni
Tokeo la picha la Eric Arnaud Otogo-Castane image
Eric Arnaud Otogo-Castane [Gabon]
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment