Magoli ya Jordy Clasie na Ryan Bertrand yameitupa nje Arsenal kwenye
kombe la EFL na kuipeleka Southampton hatua ya nusu fainali kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1987.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye hajawahi kutwaa taji hilo
katika miaka yake 20 aliyoishi London, alifanya mabadiliko ya wachezaji
10 kwenye kikosi cha Arsenal kilichoshinda 3-1 dhidi ya Bournemouth
kwenye mchezo wa Premier League Jumapili iliyopita.
Southampton ambao wameshinda mara moja katika michezo 23 waliyosafiri
kuifata Arsena, walistahili ushindi na watacheza dhidi ya Liverpool
kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa kwenye uwanja wa
St Mary January 9 mwaka ujao.
0 Maoni:
Post a Comment