LEO
REFA Kevin Friend ataonyesha kama ni rafiki au la wakati akiwasilisha
Ripoti yake ya Mechi aliyochezesha Jumamosi kati ya Manchester United na
Bournemouth huko Old Trafford na kuishia kwa Sare ya 1-1.
Mbali
ya Zlatan Ibrahimovic kukosa Penati katika Mechi hiyo iliyojaa matukio
mengi ikiwemo la Refa huyo kutoa Kadi ya Njano kwa Mchezaji wa
Bournemouth Andrew Surman na ‘kusahau’ kuwa hiyo ni Kadi ya Njano ya
Pili na kupita Dakika kadhaa ndipo ‘alipokumbuka’ na hivyo kumuwasha
Kadi Nyekundu, tukio kubwa ni ‘vita’ kati ya Sentahafu wa Bournemouth
Tyrone Mings na Straika wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic.
Vita hiyo ilifikia wakati Refa Kevin Friend kuwaonya wote Wawili lakini ikafikia kilele pale Mings alipomtimba Kichwani Ibrahimovic aliekuwa ameanguka katika Dakika ya 44 na Dakika 2 baadae Ibrahimovic alionekana ‘kumpiga kiwiko’ Mings wakati akipiga Kichwa Mpira wa Kona.
Wachezaji wote hao Wawili wamejitetea kuwa matukio hayo si ya kusudi.
Lakini kinachofuatia ni nini kimeandikwa kwenye Ripoti ya Refa Friend ambayo Leo itatua Mezani kwa FA, Chama cha Soka England.
Ikiwa
Refa huyo atakiri kuwa aliyaona Matukio hayo Mawili basi stori
inakwisha hapohapo kwani FA hawawezi tena kuchukua hatua zaidi.
Lakini
ikiwa Refa Friend atakuwa si rafiki tena akidai hakuyaona au kutotaja
chochote kwenye Ripoti yake basi FA, kwa mujibu wa Kanuni, wanaweza
kuamua kupeleka Matukio hayo Mawili kwa Jopo Huru la Marefa wa Zamani
Watatu ambao watayapitia na kuamua kama yalistahili Kadi Nyekundu au la.
Wakiamua ni Kadi Nyekundu basi FA itatoa Kifungo cha Mechi 3 au zaidi ikitegemea uzito wa kila Kosa.
Ikiwa
atafungiwa basi Ibrahimovic atazikosa Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP
dhidi ya Chelsea na Mechi za Ligi dhidi ya Middlesbrough na West
Bromwich Albion.
0 Maoni:
Post a Comment