EUROPA LIGI - ROSTOV VS MANCHESTER: MOURINHO APONDA UWANJA MBOVU WA KUCHEZEA!

 Tokeo la picha la MANCHESTER UNITED VS ROSTOV IMAGE MATCH PREVIEW

MANCHESTER UNITED wapo huko Russia kucheza Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI dhidi ya FC Rostov lakini Meneja wao Jose Mourinho ameponda hali ya Kiwanja cha Kuchezea cha Olimp-2 Stadium.
 
Uwanja huo haujatumika kwa Miezi kadhaa sasa kutokana na Ligi Kuu Russia kusimama kwa ajili ya Vakesheni ya Majira ya Baridi.
 
Mourinho amedai haupaswi kuchezewa kitu ambacho hata Kocha Mkuu wa Rostov, Ivan Daniliants, amekiunga mkono.
 
Daniliants ameeleza: "Uwanja utakuwa sawa kwa kila Mtu lakini ni tatizo!"
 
IMG-20170309-WA0001 
Hii ni mara ya kwanza kwa Man United na FC Rostov kukutana na Mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na Rekodi nzuri ya Warusi hao Uwanjani kwao.
 
Msimu huu, walipokuwa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kabla kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi lao na kutupwa EUROPA LIGI, Rostov waliinyuka Bayern Munich 3-2 hapo hapo Olimp-2 Stadium.
 
Pia Uwanjani hapo, kwenye Raundi iliyopita ya EUROPA LIGI, Rostov waliibandika Sparta Prague 4-0.
Lakini Warusi hao wanakutana na Man United yenye ngome imara ambayo haijaruhusu hata Bao 1 katika Mechi zao 4 zilizopita za Mashindano haya na pia kutofungwa Bao katika Mechi zao 6 kati ya 9 zilizopita za Mashindano yote.
 
Kwa upande wa Ufungaji Man United imepiga Bao katika kila Mechi isipokuwa Mechi 1 tu kati ya 28 walizocheza.
 
KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI:
 
De Gea, Romero, O'Hara; Valencia, Jones, Rojo, Smalling, Blind, Darmian, Young; Carrick, Herrera, Fellaini, Pogba, Mata, Lingard, Mkhitaryan; Martial, Rashford, Ibrahimovic.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment