MABINGWA wa Spain FC Barcelona Jana waliweka Historia mpya baada ya
kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, kwa kishindo kikuu
walipoitwanga Paris Saint Germain huko Nou Camp Jijini Barcelona.
Barca walichapwa 4-0 na PSG katika Mechi ya Kwanza ya Mtoano ya
Timu 16 Wiki 3 zilizopita huko Paris na haijapata kutokea katika
Historia ya UCL kwa Timu kupindua kipigo hicho na kusonga.
Lakini Jana Barca walivunja mwiko huo kwa Bao za Luis Suárez (3'),
Kurzawa (40', kajifunga mwenyewe), Messi (50', Penati), Neymar (88' na
90'+1 Penati), Sergi (90'+5 ).
Bao pekee la PSG lilifungwa na Edinson Cavani katika Dakika ya 62. Kwa Matokeo hayo Barca imesonga kwa Jumla ya Mabao 6-5 kwa Mechi 2.
0 Maoni:
Post a Comment