Licha ya ushindi mujarabu wa 2-1 dhidi ya Monaco, kocha wa Juventus
Massimilliano Allegri amekataa pongezi za aina yoyote na kusema kufanya
vizuri ni wajibu wake .
Allegri ambaye ameipa ushindi mnono Juventus kwa jumla ya goli 4-1
kwa michezo yote miwili ya nusu fainali kwenda fainali ya klabu bingwa
ulaya, amekwenda mbali zaidi na kusema anapenda kufundisha na anapenda
matokeo mazuri lakini hapendi kusifiwa pale anapotimiza wajibu wake.
”Mi kwa imani yangu pongezi zifanyike kwa mtu au jambo ambalo lina
asili ya uajabu lakini sio majukumu ya msingi ya mtu” alieleza kocha
huyo ambaye anasifika kwa misimamo mikali.
“I try to do my work serenely and with enthusiasm, but I’m not
interested in the others saying that I’m the best. I really enjoy
coaching, it helps me relax and when it starts to cause me stress, I
will stop.”
Wakati anawasili Juventus mwaka 2014 mashabiki wa timu hiyo hawakuwa
na mapenzi nae na walimkaribisha kishingo upande akitoka kufungwa na
wababe wa Italy AC Milan.
Allegri alikuja Juventus kuchukua nafasi ya Antonie Conte. Msimu wa
kwanza na Juventus mashabiki wakiwa hawamtaki aliwashangaza kwa ushindi
wa kombe la ligi na kuwapeleka michuano ya klabu bingwa ulaya akifanya
hivyo mara mbili jambo lililoanza kumfanya apendwe na mashabiki hao na
siku zote yeye akikataa sifa zao na kusema ubora wa timu ni sehemu ya
majukumu yake .
”wasifuni wachezaji kuelewa mbinu zangu na kuipa mafanikio timu yenu. Sifa kwangu hazina maana yoyote bali niombeeni tu niendelee
kutekeleza majukumu yangu katika ubora wake” alieleza kocha huyo.
Kukataa sifa na kusimamia misimamo yake pia kutojisifu mbele ya
vyombo vya habari humfanya Allegri kuwa kocha wa kipekee na kivutio kwa
wengi.
0 Maoni:
Post a Comment