MANCHESTER UNITED imetangaza kuubadili Uwanja wao wa Old Trafford ili kuruhusu Walemavu wengi kupata nafasi ya kuingia Uwanjani.
Mipango
hiyo itafanya uwezo wa Uwanja huo mkubwa kabisa England kupita Klabu
yeyote kushuka kutoka Watu zaidi ya 75,000 na kuwa takriban Watu 73,300.
Taarifa
hiyo imetamka kuwa ukarabati kamili kuwezesha Walemavu kuingia ndani
Uwanjani kirahisi ambao kwa sasa upo Jukwaa la Mashariki tu ukipanuliwa
na kuwa hadi Majukwaa ya Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton.
Lakini
mipango hiyo itaathiri baadhi ya Washabiki wa Man United wenye Tiketi
za Msimu mzima kuingia Old Trafford ambao watalazimika kuhamishiwa
maeneo mengine Uwanja hapo huku wakipewa fidia ya kuona Mechi za Makombe
bure.
0 Maoni:
Post a Comment