KATIKA soka
sasa stori kubwa hasa nchini Uingereza ni mfumo wa 3-4-3 unaoonekana
kuipa matokeo mazuri klabu ya Chelsea. Basi leo tutauangalia kidogo
mfumo huo tupate kuufahamu hapa.
Kwa asili huu
ni mfumo ambao waingereza wanasema <very offensive mind> yaani
wakushambulia zaidi ambao asili yake ni huko Uholanzi 1970 katika klabu
ya Ajax.
Walianzisha
mfumo huu kwa lengo la kutoa fursa ya kushambulia katika maumbo tofauti
tofauti. Unaweza kuwa Flat 3-4-3 au diamond 3-4-3 au wowote ambao
utatokana na kocha mwenyewe.
ULINZI
MFUMO wa 3-4-3
unaifanya safu ya ulinzi kuwa imara sana ikiwa na mabeki wa tatu dhidi
ya washambuliaji wa kati lakini unaweza kufanya mpinzani apate nafasi
hasa pembeni kama hakuna watu wazuri wakuziba nafasi hizo.
Hivyo mfumo
huo unataka kiungo mkabaji mzuri pia awe anaasili ya ku-hold/kutunza
mipira isipotee hovyo ili kuwalinda mabeki na kuongeza kuwa mabeki wanne
pindi inapohitajika.
Lakini pia inataka washambuliaji wa pembeni wazuri wanaoweza kuziba nafasi za pembeni na kupandisha mashambulizi.
Diagram A
Kiungo X8 anapaswa kuwa mkabaji sana na mlinzi wakati X4 ni mchukua mipira na kuipeleka mbele/mchezeshaji.
Pembeni viungo
X6 na X7 kazi yao ni kutoa msaada mbele kwenye mashambulizi lakini pia
kurudi nyuma zaidi kuongeza walinzi na X8 ataziba nafasi ya kati.
Ushambuliaji katika 3-4-3
Mfumo wa 3-4-3unatoa nafasi kwa timu kuwa na washambuliaji watatu.
Hivyo kwa
sababu ya kuwa na washambuliaji watatu kunawapa nafasi ya kuwa na
wachezaji wengi ambao wengine wanaweza kuwa katika nafasi ya kupokea
pasi za kupitishwa nyuma ya mabeki a.k.a through passs.
Wakati X9
anatoa cross basi X10 anakuwa mbele ya goli ili kutia presha na X11
anakuwa mkimbiaji mwenye kutafuta nafasi ya goli mara nyingi anakuwa
huru mfano Eden Hazard kwa Chelsea.
Ubora wa mfumo:
- Washambuliaji mara nyingi wanakuwa mbele kutafuta goli.
- Viungo anne wanatoa uhai kwa timu katikati na hata mbele na nyuma.
- Washambuliaji na viungo wanaweza kuchezesha timu kila upande na kuwachanga wapinzani wao hasa mabeki wasijue wakumkaba.
- Walinzi wanakuwa imara sana dhidi ya washambuliaji wa kati.
Udhaifu wa mfumo:
- Huu mfumo wa kujipanga kama umbo la almasi maarufu kama The diamond midfield formation unaweza kutoa nafasi kwa timu nyingine kuzitumia kutokana na kuwa gaps nyingi endapo hakuna wachezaji wanaoendana na mfumo huu.
- Mabeki au walinzi wakiwa watatu wanaweza kuwa rahisi kuchanganywa na wachezaji wenye kasi wanaobadilishana nafasi.
Mahitaji ya mfumo
- Mabeki wenye kasi na wenye uwezo kimwili na kiafya kuziba nafasi ya beki wanne.
- Viungo wakabaji wazuri wenye kuwa na uwezo wa kuzuia mipira ya mashambulizi ya kushtukiza pia waporaji wazuri wa mipira.
- Washambuliaji wenye kuweza kuendesha mipira mbele ikiwezekana kasi na uwezo binafsi wakupunguza walinzi pindi inapohitajika.
- Zaidi ni mawasiliano mazuir kati ya walinzi na viungo ili kuwa na ulinzi mzuri.
0 Maoni:
Post a Comment