Kocha wa timu ya soka ya taifa ya
wanawake, Twiga Stars, Sebastian Nkoma ameita wachezaji 45 kwa ajili ya
mchujo wa kupata nafasi ya kujiunga na kikosi cha timu hiyo
kitakachoshiriki mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
Ghana mwaka 2018.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba
wachezaji hao wataingia kambini Mei 21 hadi 27 kwa ajili ya kuangaliwa
na watakaoonyesha uwezo watachukuliwa kikosi cha Twiga Stars.
Madadi,
kocha wa zamani wa klabu ya Simba, amesema kwamba baada ya kupatikana
wachezaji wa kuongezwa Twiga Stars, kambi rasmi ya maandalizi ya mechi
za kufuzu AFCON ya Ghana mwakani itaanza Septemba au Oktoba, mwaka huu.
Amesema lengo si kukata titeti ya kushiriki fainali za AFCON za Ghana
tu, bali pia na kupata nafasi ya kwenda Kombe la Wanawake Ufaransa mwaka
2019.
Wachezaji walioteuliwa na kocha Sebastian Nkoma kwa ajili
ya kuwania nafasi ya kuingia kikosi cha Twiga Stars kufuatia kufanya
vizuri kwenye Ligi Kuu ya Taifa miezi miwili iliyopita ni;
Agatha Joel,
Ever Jackson, Christina Daudi, Shamim Khamis, Saada Ramadhani, Oprah
Clement, Faraja Kimula, Zubeda Juma, Irene Mkundila, Veronica Mazanda,
Christina Pangrasi, Aisha Hamza, Emil Mdim, Semeni Hussein na Mgeni
Kisuda.
Wengine ni Daclina Mwisigao, Esther Mayala, Enekia Yona,
Herieth Shijja, Janeth Petro, Arafa Omar, Elizabeth Nashon, Zainab
Abdallah, Rehema Butene, Zainab Mlenda, Hadija Mohammed, Grace Mbelay,
Aquila Gasper, Shan Sultan na Rukia Anafi.
Wengine ni Zuena Aziz,
Amina Ramadhani, Neema Paul, Rehema Abdul, Kapangara Kingamkono, Asha
Malaigwa, Antoneka Mbunga, Sylvia Mwacha, Aisha Mbabaje, Rukia Magi,
Hawa Suleiman, Amina Abdallah, Saida Muhaji, Mwamvita Muba na Oliver
Lyimo.
KILA LA KHERI TWIGA STARS
Kila la kheri timu yetu katika kuchagua kikosi imara na cha ushindani
ReplyDelete