Wachezaji watano wameteuliwa
kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa
2016/2017.
Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi
Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba),
Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Majina hayo
yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za
Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini.
Wahusika watatumiwa fomu maalum za
kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari.
Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.
Hafla
ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu
kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
0 Maoni:
Post a Comment