PLUIJM ATAKA KUANZA KUONYESHA MAJONJO YAKE SPORTPESA SUPER CUP


Kikosi cha Singida United kitaendelea na mazoezi yake leo kujiandaa na michuano ya Sport Pesa Super Cup.

Kocha Mkuu wa Singida United, Hans van der Pluijm, amesema michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara lakini kutengeneza morali ya kikosi chake.


“Kuna mabingwa wa ligi kuu, mabingwa wa kombe la shirikisho. Lakini kuna timu kutoka Kenya, haitakuwa michuano rahisi kwa timu mpya kama yetu.

“Lakini tunataka kucheza soka safi na la ushindani na kushinda ili kujenga morali lakini kuendelea kujenga kikosi chetu kabla ya ligi kuu ukiwa ni msimu wa kwanza,” alisema Pluijm.

Timu nyingine za Tanzania Bara zilizo katika michuano hiyo ni Simba na Yanga wakati Jang’ombe inatokea Zanzibar.


Timu kutoka Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment