Mlinzi wa zamani wa klabu ya Arsenal
Martin Keown amesema kuwa meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger anapaswa
kuwauza nyota wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil baada ya kuongeza muda
wa kusalia kuinoa miamba hiyo ya London.
Mfaransa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na amesema kuwa timu yake inaweza kupigana na kutwaa ubingwa msimu ujao.
Viungo Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa pamoja wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa mwaka huu.
Keown
anasema kuliko kupata hasara ya kuwaruhusu kuondoka bure ni vyema
akafanya maamuzi magumu ya kuwauza nyota hao na kutengeneza faida
itakayoweza kuleta wachezaji wapya na wenye morali kubwa zaidi.
Sanchez amefunga magoli 24 na kuchangia kupatikana
kwa mengine 10 huku Ozil akifunga nane na kuchangia tisa lakini hiyo
haikutosha kuifanya timu hiyo kukosa michuano ya mabingwa wa Ulaya msimu
ujao jambo ambalo linatia ukakasi kwa Sanchez na Ozil kuongeza mikataba
yao.
Sanchez amepewa ofa ya paundi 300,000 kwa wiki lakini bado hajasaini mkataba huo, huku Ozil akikataa paundi 250,000 kwa wiki.
0 Maoni:
Post a Comment