Vyombo vya habari nchini Brazil
vinasema kuwa mifupa ya gwiji wa zamani wa soka nchini humo Manuel
Francisco dos Santos maarufu kama Garrincha, inaweza kuwa imepotea zaidi
ya miongo mitatu baada ya kifo chake akiwa na miaka 49.
Kuna
makaburi mawili ambayo yote yana majina yake mjini Rio de Janeiro lakini
inawezekana kati ya hayo hakuna hata moja ambalo ni lake.
Mmoja wa wahifadhi wa makaburi hayo anasema kuwa
mifupa yake inaweza kuwa ilihamishwa miaka kadhaa iliyopita ila
haijulikani wapi haswa ilipelekwa.
Garrincha mpinzani mkubwa wa
Pele wa ni nani zaidi katika historia ya soka kwa nchi hiyo, aliisaidia
nchi yake kutwaa kombe la dunia mwaka 1958 na 1962.
0 Maoni:
Post a Comment