JANA Mabingwa wa Italy Juventus wamebeba Coppa Italia kwa mara ya
12 ikiwa ni Rekodi kwa kuichapa Lazio 2-0 kwenye Fainali iliyochezwa
Stadio Olimpico Jijini Rome huko Nchini Italy.
Kwa kubeba Kombe hili Juve sasa wamekamilisha awamu ya kwanza ya
Trebo Msimu huu kwani Wikiendi hii inayokuja wanaweza kutetea vyema
Ubingwa wao wa Serie A kwa mara ya 6 mfululizo na hapo Juni 3 wanaweza
kutwaa Ubingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwafunga Mabingwa Watetezi Real
Madrid huko Cardiff, Wales.
Jana Bao za ushindi za Juve zilifungwa na Mabeki wao Dani Alves Dakika ya 12 na Leonardo Bonucci katika Dakika ya 24.
Juve, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, wamekuwa Timu ya kwanza kubeba Coppa Italia mara 3 mfululizo.
Kwa Lazio hii ilikuwa ni Fainali yao ya 3 katika Miaka Mitano.
0 Maoni:
Post a Comment