Kikosi cha Yanga kinarejea uwanjani leo kuanza maandalizi ya mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara.
Wachezaj hao watarejea mazoezini leo na
kuanza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa, hii ikiwa ni baada ya
mapumziko ya siku moja.
Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja ikiwa ni baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Toto African.
Yanga iko kileleni mwa ligi ikiwa imejihakikishia ubingwa huku Simba wakiamini watafanya miujiza.
Miujiza wanayosubiri Simba ni kushinda
mechi ya mwisho kwa zaidi ya mabao matano dhidi ya Mwadui FC na Yanga
wafungwe na Mbao FC ikiwezekana zaidi ya mabao matatu.
0 Maoni:
Post a Comment