PENATI
YA Dakika ya 30 iliyofungwa na Andre Ayew imewapa Ghana ushindi wa Bao
1-0 walipocheza na Uganda katika Mechi ya Kundi D la AFCON 2017,
Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, iliyochezwa
Stade de Port Gentil Mjini Port Gentil Nchini Gabon.
Penati
hiyo ilitolewa baada ya Isaac Isinde kumvuta Harrison Afful ndani ya
Boksi na Andre Ayew, Mchezaji wa Klabu ya West Ham huko England kumfunga
Kipa na Mchezaji Bora Afrika Dennis Onyango.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Uganda kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika tangu 1978 ambazo walifungwa Mechi ya mwisho kabisa, Fainali, na
Wenyeji wa Fainali hizo Ghana.
Mechi ya Pili ya Kundi D ilichezwa kati ya Mali na Egypt, ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutokufungana.
Leo Jumatano ni Mechi za Pili za Kundi A ambapo Wenyeji Gabon watacheza na Burkina Faso na Vigogo Cameroon kuwavaa wapya wa Mashindano haya Guinea-Bissau.
VIKOSI VILIVYOANZA:
GHANA: Braimah
Razak, Abdul Rahman Baba [Acheampong 39'], Harrison Afful, Daniel
Amartey, John Boye, Mubarak Wakaso, Thomas Teye Partey, Jordan Pierre
Ayew [Acquah 85'], Andre Ayew, Christian Atsu, Asamoah Gyan [Badu 72']
UGANDA: Dennis
Onyango, Dennis Iguma, Joseph Ochaya, Isaac Isinde [Serunkuma 70'],
Hassan Wasswa Mawanda, Tonny Mawejje, Geofrey ‘Baba’ Kizito, Michael
Azira [Oloya 45'], Faruku Miya, William Luwaga Kizito [Shaban 57'],
Geoffrey Massa.
Joshua Bondo [Botswana] |
0 Maoni:
Post a Comment