TIMU ZA DARAJA LA CHINI ZAPETA EMIRATES FA CUP 2017.

 Tokeo la picha la EMIRATES FA CUP IMAGE
Jana katika Mechi za Marudiano za Raundi ya 3 ya EMIRATES FA CUP, Klabu za Madaraja ya chini Lincoln na Sutton zilishangaza Dunia kwa kuzibwaga Klabu za Madaraja ya juu yao na kusonga Raundi ya 4.
 
Leo, huko Home Park, Klabu ya Daraja la Ligi 2, Plymouth Argyle, ikiwa ipo Madaraja Matatu chini ya EPL, Ligi Kuu England, inarudiana na Vigogo Liverpool baada kutoka 0-0 huko Anfield katika Mechi ya Raundi ya 3.
 
Jana, Christian Benteke alimnusuru Meneja wake Sam Allardyce na kumpa ushindi wake wa kwanza tangu achukue mamlaka baada kutoka Benchi na kupiga Bao 2 walipokuwa nyuma 1-0 na kuipa Crystal Palace ushindi wa 2-1 dhidi ya Bolton Wanderers na kutinga Raundi ya 4 ambapo watakuwa Nyumbani kucheza na Man City.
 
Nao Lincoln, wanaocheza Ligi ambayo si rasmi, wameitoa Timu ya Daraja la Pili, Daraja la Championship, Ipswich Town 1-0 na kuingia Raundi ya 4 ambayo watacheza Nyumbani na Brighton & Hove Albion.             

JE WAJUA?
  • FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
  • Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
  • Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
  • Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
  • Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

Sutton, ambao wako Daraja la 5, pia wameleta maajabu kwa kuibwaga Timu ya Daraja la 3 AFC Wimbledon Bao 3-1 na kusonga Raundi ya 4 ambako watacheza Nyumbani na Timu ya Daraja la Championship Leeds United.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment