MECHI za Raundi ya 6 ya EMIRATES FA CUP, ambayo ndiyo Robo Fainali, zitachezwa Machi 11 na moja ya mvuto mkubwa ni Mabingwa Watetezi Manchester United kutua Stamford Bridge kupambana na Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea.
Hiyo ndio Bigi Mechi pekee kwenye Raundi hiyo wakati Mechi nyingine zikipambanisha ‘Timu kubwa’ na upinzani hafifu.
Lakini, ikiwa Man City wataitoa Huddersfield katika Mechi yao ya Marudiano ya Raundi ya 5 kufuatia Sare ya 0-0 basi watakuwa Wageni wa Middlesbrough na hii itakuwa ni Mechi ya Pili kukutanisha Timu za EPL, Ligi Kuu England, baada ya ile kati ya Chelsea na Man United.
JE WAJUA?
- FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwa na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
- Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
- Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
- Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
- Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
Arsenal wao watakuwa Nyumbani Emirates kucheza na Lincoln City, Timu ambayo haipo Mfumo rasmi wa Ligi huko England, ambayo ilijizolea sifa kubwa kwa kuibwaga Burnley wanaocheza EPL na waliokuwa Nyumbani kwao.
FA CUP
Ratiba
Jumatano Machi 1
Raundi ya 5 - Marudiano
2245 Manchester City v Huddersfield Town [Mechi ya Kwanza 0-0]
Jumamosi Machi 11
Raundi ya 6 [Robo Fainali]
#### Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni ###
Arsenal v Lincoln City
Chelsea v Manchester United
Middlesbrough v Huddersfield/Man City
Tottenham Hotspur v Millwall
0 Maoni:
Post a Comment