Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, zilizoanza kwa kishindo Wiki iliyopita kwa Vigogo Barcelona kunyukwa 4-0 na Arsenal kushindiliwa 5-1, Jana zimeendelea tena kwa Mechi mbili zilizozaa Magoli kibao.
Huko Etihad, Man City waliifunga kwa mbinde AS Monaco Bao 5-3 na hadi Mapumziko Monaco walikuwa mbele 2-1 na kuna wakati waliongoza 3-2.
Magoli kwenye Mechi hiyo yalifungwa na Rahim Sterling, Dakika ya 26, Agüero, 58' na 71’, Stones, 77', na Leroy Sané, 82', kwa upande wa City na Monaco Wafungaji wao walikuwa Radamel Falcao, Dakika za 32 na 61, na jingine ni Mbappe, 40'.
Huko Germany, Bayer 04 Leverkusen walichapwa 4-2 na Wageni wao Atlético Madrid.
Wafungajji wa Mechi hiyo kwa Leverkusen ni Bellarabi, Dakika ya 48 na Savic, 67' kajifunga mwenyewe, huku Atletico wakipiga kupitia Ñíguez, 17', Griezmann, 25', Gameiro, 58', na Penati ya Dakika ya 86 ya Fernando, Torres.
Leo Jumatano zipo Mechi mbili kwa FC Porto kuikaribisha Juventus huko Ureno na Sevilla ya Spain kuwa Mwenyeji wa Mabingwa wa England Leicester City ambao Msimu huu wameparaganyika.
Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya yataanza Jumanne Machi 7.
0 Maoni:
Post a Comment