UEFA EUROPA LIGI: LEO MAN UNITED KUIRUDIA SAINT-ETIENNE.

>>JE WAJUA KWANINI MECHI HII INAPIGWA LEO BADALA YA ALHAMISI?
Tokeo la picha la man u image europa league
Manchester United Usiku huu wapo Stade Geoffroy Guichard Uwanja wa Jijini Saint Etienne Nchini France unaopakia Washabiki 42,000 kurudiana na Saint-Etienne katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Alhamisi iliyopita huko Old Trafford Man United waliichabanga Saint-Etienne 3-0 kwa Hetitriki ya Zlatan Ibrahimovic huku mvuto mkubwa ukiwa kupambanishwa kwa Mtu na Kaka yake Paul Pogba wa Man United na Kaka MkubwaFlorentin Pogba Beki wa Saintt-Etienne ambae hata hivyo hakudumu Dakika 90 baada ya kuumia Dakika ya 79 na kubadilishwa huku Mdogo Mtu akikosa Bao kadhaa na kupiga Posti pia.

JE WAJUA?
  • Kwanini Mechi hii inachezwa Leo Jumatano badala ya Usiku wa EUROPA LIGI Alhamisi?
  • Sababu ni kuwa Wapinzani wakubwa wa Saint-Etienne, Lyon, nao Alhamisi Usiku wapo kwao kucheza na AZ Alkmaar pia kwenye EUROPA LIGI.
  • Kutokana na Timu hizo pinzani kuwa Jirani, wakitenganishwa na umbali wa takriban Kilomita 50 tu, Mechi ya Saint-Etienne na Man United ikavutwa kuwekwa Jumatano badala ya Alhamisi kamili ilivyo desturi.


Hali za Vikosi.
Jose Mourinho amethibitisha Wayne Rooney na Phil Jones hawapo fiti huku pia Kiungo Ander Herrera akikosekana baada ya kulimbikiza Kadi za Njano 3 na hivyo kufungiwa Mechi 1
Baada ya Timu hizi kukutana Alhamisi iliyopita, Man United Jumapili iliichapa Blackburn Rovers 2-1 kwenye FA CUP na kutinga Robo Fainali wakati Saint-Etienne wakichapwa na Montpellier huko France.
Hatari
Straika wa Man United, Zlatan Ibrahimovic, Jumapili alifunga Bao la ushindi dhidi ya Blackburn Rovers na hilo lilikuwa Bao lake la 24 kwa Msimu huu na pia ni la 18 katika Mechi zake 20 zilizopita.
Lakini Takwimu kubwa ni kuwa Ibrahimovic amefunga Bao 17 katika Mechi 14 dhidi ya Saint-Etienne, mengine yakiwa ni yale alipokuwa akiichezea Paris Saint-Germain.
Nyingine.
Mbali ya Mechi hiyo ya Saint-Etienne na Man United hapo Jumatano, Siku hiyo pia zipo Mechi nyingine 2 za Marudiano Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI na zilizobakia kuchezwa Alhamisi kama ilivyo ada.
Washindi wa Mechi hizi watatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watajua Wapinzani wao baada ya kufanyika Droo yake hapo Ijumaa February 24 huko Nyon, Uswisi.
KIKOSI CHA MAN UNITED KILICHOENDA FRANCE:
De Gea, O'Hara, Romero; Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling, Valencia, Young; Carrick, Fellaini, Mata, Mkhitaryan, Pogba, Lingard, Schweinsteiger; Ibrahimovic, Martial, Rashford. 
REFA: Deniz Aytekin (Germany)
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment