Jose Mourinho amewaambia mashabiki wake kwamba mechi ya Jumapili dhidi ya
Liverpool haitakuwa ''matembezi ya ukumbi wa filamu' na badala yake
ameitaka Liverpool kujiandaa vilivyo.
United iliishinda Hull City
2-0 katika awamu ya kwanza ya mechi ya kombe la Ligi EFL siku ya
Jumapili kufuatia mabao ya Juan Mata na Marouane Fellaini yaliotikisa
wavu.
Hata hivyo Mourinho amesema kuwa kila mchezaji anafaa kufanya kazi ya ziada dhidi ya Liverpool.
''Ni mechi muhimu sana kwetu, alisema.Tunapocheza vyema mashabiki pia hushirikiana nasi .
Tunaposhindwa kucheza vizuri ni vyema kwamba mashabiki hawapaswi kulalamika sana.
Kila
mtu anapenda mechi kubwa, wachezaji,wakufunzi na mashabiki. Kila mmoja
anapenda mechi kubwa kwa hivyo tuelekee katika mechi hiyo siku ya
Jumapili''.
Liverpool imepoteza mara mbili pekee msimu huu ,ikiwa imeshindwa 4-3 na Bournemouth mnamo tarehe 4 mwezi Disemba.
Timu
hiyo ya Jurgen Klopp ni ya pili katika ligi ya Uingereza, ikiwa pointi
tano mbele ya United iliopo katika nafasi ya sita na pointi tano nyuma
ya viongozi wa ligi Chelsea.
0 Maoni:
Post a Comment