Kazuyoshi Miura mchezaji
raia wa Japan anayecheza katika klabu ya Yokohama ameendelea kufunga
ingawa amekuwa ni mchezaji mwenye umri mkubwa sana katika ligi ya nchini
Japan,
Miura ambaye amefunga
akiwa na umri wa miaka 49 amefikisha umri wa miaka umri wa 50 mwezi wa
Februari amefanikiwa kuongeza mkataba mpya na timu yake huku akisubiria
msimu mpya unaoanza mwezi wa pili.
Miura ambaye amewahi kucheza barani ulaya amecheza mechi 89 kwa Japan akiifungia magoli 55.
Miura ataitumikia klabu
ya Yokohama katika msimu ujao ambao kwake atakuwa ni msimu wa 32 katika
mpira wa kulipiwa. Miura alistaafu kuchezea soka miaka 17 iliyopita na
hivyo nguvu zake nyingi anazitumia kwa klabu yake ya Yokohama.
Kutokana na Miura kuwa
na umri huo atakuwa anaingia kwenye list ya wachezaji wengi wenye umri
mkubwa Duniani huku umri mkubwa zaidi ukiwa ni mika 53.
0 Maoni:
Post a Comment