www.kiungomshambuliaji.blogspot.com inakuletea; KUELEKEA
fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kesho Ijumaa, Kocha
Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Idd Nassor
Cheche, ameweka wazi kuwa wanajua namna ya kuikabili Simba na kupata
matokeo mazuri kwenye mchezo huo.
Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC jioni ya JANA ya kujiandaa na mchezo huo, ambapo imeingia fainali baada ya
kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo
Frank Domayo.
“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano
hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi
tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi
kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama
tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche wakati
akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz
AZAM FC FIRST TEAM. |
Alisema katika mazoezi ya kwanza wachezaji wa kikosi hicho wameyaanza
vema wakiwa na furaha na mwanzo mpya huku akidai kuwa licha ya
ushindani utakaoonyeshwa kwenye mchezo huo wamejipanga kukabiliana na
hali hiyo.
Cheche ambaye atakiongoza kikosi hicho kama kocha mkuu hadi
kumalizika kwa michuano hiyo kabla ya kumpisha Kocha Mkuu mpya wa Azam
FC aliyetambulishwa jana, Aristica Cioaba raia wa Romania, mpaka sasa
amekiongoza kikosi hicho kuandika rekodi ya aina yake ya kutofungwa
mchezo wowote wala kuruhusu bao.
Hadi inaingia fainali kwa kuitoa Taifa ya Jang’ombe, Azam FC kwenye
hatua ya makundi iliichapa Zimamoto bao 1-0, ikatoa suluhu na Jamhuri
kabla ya kuifumua Yanga mabao 4-0, ukiwa ni ushindi wa kihistoria tokea
timu hizo zianze kukutana.
Azam FC LEO Alhamisi jioni itamalizia mazoezi yake ya mwisho kabla
ya kuivaa Simba kwenye mchezo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na
mamilioni ya Watanzania wapenzi wa soka.
0 Maoni:
Post a Comment