Manchester City wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka
England, kwa kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu huku
Wapinzani wao Manchester United wakiripotiwa kuanzisha mchakato wa
kuongeza Mkataba wa Kiungo wao Marouane Fellaini.
CITY NA PILATO WA FA
Manchester City wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu.
City wamepewa hadi Januari 19 kujibu Mashitaka hayo.
Imedaiwa kuwa City walishindwa kuwapa Taarifa Maafisa wanaopima Wachezaji Matumizi ya Madawa Haramu.
Kila Klabu hupaswa kujulisha Wachezaji wao watakuwa wapi kwa ajili
ya kupimwa lakini City walishindwa kutoa Taarifa za Ratiba ya Mazoezi na
wapi Wachezaji hao watapatikana baada ya Mazoezi ili Maafisa husika wajue wakati wote wapi watawapata wakitakiwa kupimwa.
Imedaiwa City ilishindwa mara 3 kupeleka Taarifa za waliko Wachezaji wao na ndio maana FA imewashitaki. Kawaida kosa kama hilo huadhibiwa kwa Faini.
UNITED KUMWONGEZEA FELLAINI!
Manchester United wameripotiwa kuanzisha mchakato wa kuongeza
Mkataba wa Kiungo wao Marouane Fellaini ili kumbakisha Old Trafford hadi
Mwaka 2018.
Fellaini alijiunga na Man United Mwaka 2013 akitoka Everton kwa Dau
la Pauni Milioni 27.5 na kusaini Mkataba wa Miaka Minne ukiwa na
Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Mwezi uliopita Fellaini alizomewa na Mashabiki wa Man United lakini
Juzi alipiga Bao la Pili wakati Man United inaichapa Hull City 2-0
ndani ya Old Trafford katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP.
Mara baada kupachika Bao hilo, Fellaini, mwenye Miaka 29,
alimkimbilia Mourinho na kumkumbatia kwa furaha na pia kuonyesha shukran
kwa Meneja wake kwa kumsapoti kwenye kipindi kigumu akisakamwa na
Mashabiki baada kusababisha Penati iliyowapa Everton Sare Mwezi Desemba.
Akiongea mara baada ya kuwafunga Hull City Juzi, Mourinho alinena:
"Yeye ana moyo mgumu na amestahamili vizuri. Anajijua kwamba yeye ni
Mchezaji muhimu kwangu!"
0 Maoni:
Post a Comment