BAADA YA KUSIMAMA KWA EPL tangu Januari 4 wakati Tottenham Hotspur ilipowatandika Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Bao 2-0, Ligi hii inarejea tena Wikiendi hii.
Mechi
ya kwanza kabisa ni Jumamosi huko White Hart Lane ambako Spurs, walio
Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya Pili Liverpool na 7 nyuma
ya Chelsea, watacheza na West Bromwich Albion walio Nafasi ya 8.
Kisha
Siku hiyo hiyo Jumamosi zitafuata Mechi 6 zote zikianza Saa 12 Jioni na
kati ya hizo ni ile ya Swansea City, ambao wako Nafasi 1 toka mkiani,
kuwakaribisha Arsenal walio Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Vinara
Chelsea.
Siku
hiyo, Mechi ya mwisho ni Usiku huko King Power Stadium ambako Mabingwa
Watetezi Leicester City watacheza na Chelsea ambao ndio wanaongoza Ligi
na ndio kwanza wakitoka kwenye kipigo cha 2-0 toka kwa Spurs.
Jumapili zipo Mechi 2 ikianza ile ya Goodison Park kati ya Everton, walio Nafasi ya 7, na Man City ambao wako Nafasi ya 4.
Kisha
utafuata mtanange huko Old Trafford wakati Man United ambao wapo kwenye
wimbi la kushinda Mechi 9 mfululizo wakicheza na Mahasimu wao wa Jadi
Liverpool.
Wimbi
hili la ushindi kwa Man United ni refu tangu Msimu wa 2008/09
waliposhinda Mechi 11 mfululizo kati ya Januari na Februari na kuelekea
kutwaa Ubingwa wa England na Kombe la Ligi wakiwa chini ya Meneja
Lejendari Sir Alex Ferguson.
EPL – Ligi Kuu England Ratiba
++Saa za Bongo++
Jumamosi Januari 14
1530 Tottenham vs West Bromwich Albion
1800 Burnley vs Southampton
1800 Hull City vs Bournemouth
1800 Sunderland vs Stoke City
1800 Swansea City vs Arsenal
1800 Watford vs Middlesbrough
1800 West Ham United vs Crystal Palace
2030 Leicester City vs Chelsea
Jumapili Januari 15
1630 Everton v Manchester City
1900 Manchester United v Liverpool
0 Maoni:
Post a Comment