MFARANSA
Dimitri Payet ameiambia Klabu yake West Ham kwamba anataka kuondoka
Januari hii kwa mujibu wa habari alizotoboa Meneja wa Klabu hiyo Slaven
Bilic.
Akiongea
na Wanahabari hii Leo kuelekea Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England,
Jumamosi na Crystal Palace, Bilic amesema Mchezaji huyo amegoma kucheza
Mechi hiyo ya Jumamosi.
Lakini
Bilic amesisitiza licha ya Mchezaji huyo alienunuliwa na West Ham Mwaka
2015 kutoka Marseille kwa Pauni Milioni 10 kukataa kucheza, Klabu yao
haina nia kumuuza.
Bilic amepasua kuwa Payet, mwenye Miaka 29, amesimamishwa kujiunga na Mazoezi ya Timu hadi sakata lake liishe.
Bilic amesema: “Hatumuuzi. Tumempa kila kitu lakini ametuangusha. Nimekasirika sana!”
Zipo
ripoti kuwa Mchezaji huyo, ambae Februari Mwaka Jana alipewa Mkataba
Mpya wa Miaka 5 na Nusu, anatakiwa huko kwao France huku Klabu za
Marseille na Paris Saint-Germain zikitajwa sana.
Bilic
mwenyewe amekiri kuwa anajua Payet amesharubuniwa na Klabu nyingine
lakini yeye hajakata tamaa kubaki kwa Mchezaji huyo hapo West Ham.
Bilic
amesema: “Natarajia atarudi na kuonyesha ari kwa Timu kama vile Timu
ilivyomwonyesha yeye. Nimeongea na Klabu, Mwenyekiti na Makamu wake. Si
suala la Fedha. Tunataka abaki!”
0 Maoni:
Post a Comment