Wakati
timu pinzani ‘derby’ za JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikitarajiwa kuchuana leo Ijumaa Januari 13, 2017 kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko
Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Bodi
ya Ligi Kuu, imetangaza tarehe rasmi za michezo mitatu ambayo awali
haikupangiwa tarehe katika ratiba.
Mbali
ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14, 2017
kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui
FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Kadhalika
siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa
Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo
mwingine wa VPL.
Jumapili
Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya Vodacom
ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kadhalika
Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako Tanzania
Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Michezo
mitatu ambayo haikupangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA ikiwa na
maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya Ligi – chombo
cha Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), kinachosimamia na kuendesha
ligi, imepanga tarahe.
Tarehe
hizo ni Januari 17, 2017 – siku ya Jumanne kutakuwa na mchezo mmoja
kati ya Majimaji itakayowaalika mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, Young Africans ya Dar es Salaam katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika
mechi nyingine ziliopangiwa tarehe na muda ni kati ya Mtibwa Sugar
itakayocheza na Simba, Jumatano Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mchezo
huu wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku wakati michezo yote
tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa
mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam
- Wadhamini wenza wa ligi hiyo.
Ligi
hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), Mdhamini
Mkuu ni Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom iliyokuza ubora wa huduma
zake hapa nchini katika mawasiliano ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi
wa maneno na intaneti yenye kasi.
VPL,
LIGI KUU VODACOM
Ratiba
- Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa
Ijumaa Januari 13
JKT Ruvu v Shooting [Mabatini, Mlandizi]
Jumamosi Januari 14
Stand United v Mwadui FC [Kambarage, Shinyanga]
Kagera Sugar v Ndanda FC [Kaitaba, Bukoba]
Jumapili, Januari 15
Mbao FC v African Lyon [CCM Kirumba, Mwanza]
Jumatatu Januari 16
Toto Africans v Tanzania Prisons [CCM Kirumba, Mwanza]
Jumanne Januari 17
Majimaji FC v Yanga [Majimaji, Songea]
Jumatano Januari 18
Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]
1900 Azam FC v Mbeya City [Chamazi, Dar es Salaam]
0 Maoni:
Post a Comment