VPL, Ligi
Kuu Vodacom, Jana imeendelea huko Uwanja wa Majima Mjini Songea wakati
Majimaji FC ilipofungwa 1-0 na Mabingwa Watetezi Yanga.
Bao la ushindi la Yanga lilipachikwa Dakika ya 14 na Deus Kaseke.
Matokeo
haya yamewaweka Yanga kuwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba ambao leo
wapo huko Jamhuri Jijini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.
Mechi nyingine ambayo pia itachezwa leo ni huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mbeya City.
0 Maoni:
Post a Comment