Timu ya taifa ya vijana chini ya
umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inarejea Uwanja wa L'Amitie mjini
Libreville kumenyana na Angola katika mchezo wake wa pili wa Kundi B
Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 zinazeondelea .
Serengeti
Boys inayofundishwa na Bakari Nyundo Shime, anayesaidiwa sana na
Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen itahitaji ushindi katika mchezo
wa leo kuweka hai matumaini ya kusonga mbele baada ya kulazimisha sare
ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza na Mali, ambayo leo itamenyana na
Niger.
Kwa ujumla timu zote za Kundi B zitakuwa zinasaka ushindi wa
kwanza leo, baada ya Angola pia kutoka sare ya 2-2 na Niger kwenye
mchezo wa kwanza.
Kundi A tayari Ghana imekuwa ya kwanza
kutinga Nusu fainali baada ya kuwafunga wenyeji, Gabon mabao 5- 0 jana
Uwanja wa Port Gentil.
Mshambuliaji na Nahodha, Eric Ayiah aliye katika
kiwango kizuri na kiungo, Emmanuel Toku kila mmoja alifunga mabao mawili, wakati Patmos Arhin aliyetokea benchi kipindi cha pili alifunga
lingine.
Matokeo hayo yanamaanisha Ghana inafikisha pointi sita
na mabao tisa baada ya Jumapili kushinda 4-0 dhidi ya Cameroon katika
mchezo wake wa kwanza.
Maana yake pia Ghana wamejikatia tiketi ya
kushiriki Fainali za Kombe la Dunia za U-17 baadaye mwaka huu, wakati
wenyeji wanapoteza nafasi ya kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza
kufungwa pia 5-1 na Guinea.
Mchezo uliotangulia wa Kundi A jana, Cameroon ilijiweka mguu nje baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Guinea.
Kwa
matokeo hayo, Guinea inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 5-1
dhidi ya wenyeji Gabon, wakati Cameroon inaokota pointi ya kwanza
kutokana na sare hiyo, baada ya awali kufungwa 4-0 na Ghana.
Mshambuliaji
wa Les Syli Cadets, Djibril Fandje Toure aliifungia bao la kuongoza
Guinea dakika ya 22 ambalo linakuwa bao lake la nne kwenye mashindano
haya, kabla ya Stephane Zobo kuisawazishia Cameroon dakika ya 67.
Kila la
heri Serengeti Boys ya Watanzania katika mchezo wa leo. Mungu ibariki
Tanzania. Mungu ibariki timu yetu ya vijana ishinde leo. Amin.
0 Maoni:
Post a Comment