BABA Mzazi wa Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amefariki Dunia akiwa na Miaka 79 baada ya kuugua.
Fassou Antoine Pogba aliihama Nchi yake Guinea kutoka Afrika na kwenda Paris, France akiwa na Miaka 30.
Mbali ya Paul Pogba, Watoto wake wengine ni Mapacha Florentin na Mathias ambao wote ni Wanasoka.
Wakati Pogba akiamua kuichezea France, Ndugu zake Florentin na Mathias wao waliamua kuiwakilisha Guinea.
Familia
ya Pogba ilithibitisha kwa Gazeti la France, Le Parisien, kuwa Mzee
Fassou Antoine Pogba, aliekuwa akiugua, alifariki Jana Ijumaa.
Mwaka
Jana kwenye Fainali za EURO 2016, Mzee Fassou alionekana Jukwaani
Uwanjani akiwa na Wanawe Florentin na Mathias wakimshangilia Paul Pogba
akiichezea France walipokutana nae Switzerland.
Mwezi Machi Pogba alitoa Picha kwenye Instagram akisheherekea Siku ya Kuzaliwa ya Baba yake na kuandika:
'Happy birthday dear Dad, I feel blessed to be your son #pogdaddy #fighter #pogbance.'
Mzee
Fassou alitua France akiwa hana hata Senti Moja lakini hakusahau Soka
lake aliloanzia huko kwao Guinea na baadae kuendelea kuwa Kocha
akiwafundisha pia Wanawe Watatu huko Roissy-en-Brie.
Mwaka
2016 alipohojiwa na Wanahabari alinena: “Nilicheza Soka Madaraja ya
chini kupita nilivyotaka. Nilitaka Wanangu wacheze Madaraja ya juu,
Nilikuwa mkali mno kwao walipokuwa wadogo na hilo liliwafanya wajifunze
haraka. Ilifika wakati nafundisha Watoto wengine ili mradi Paul aweze
kucheza akiwa na Miaka Minne, Mitano, Sita. Nilitaka wawe kiwango cha
juu kabisa!”
PUMZIKA KWA AMANI, Baba yetu.
0 Maoni:
Post a Comment