Chelsea
wametwaa Ubingwa wa England huko The Hawthorns baada ya kuitungua West
Bromwich Albion 1-0 katika Mechi ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa Bao la
Dakika ya 82 la Michy Batshuayi alietokea Benchi.
Chelsea
sasa wanaongoza Ligi hii wakibakisha Mechi 2 na wana Pointi 87 kwa
Mechi 36 ambazo haziwezi tena kufikiwa na Timu ya Pili Tottenham Hotspur
ambao wana Pointi 77 kwa Mechi 35.
Batshuayi,
Mchezaji kutoka Belgium mwenye Miaka 23, alikuwa hajaifungia Chelsea
tangu Agosti, aliingizwa Dakika ya 76 kumbadili Pedro na kuseleleka
kuunganisha Pasi ya Cesar Azpilicueta na kufunga Bao lililoipa Chelsea
Ubingwa chini ya Meneja Mpya wa Msimu huu Mtaliana Antonio Conte.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
JE WAJUA?
- Chelsea wametwaa Taji la 6 la Ubingwa England na la 5 kwenye zama hizi za EPL, Ligi Kuu England. Timu pekee iliyotwaa Mataji mengi ya Ubingwa England ya EPL ni Manchester United yenye Mataji 13 ya EPL na 20 kwa Ujumla.
- Antonio Conte ni Meneja wa 4 kutoka Italy aliewahi kutwaa Ubingwa wa England kufuatia Carlo Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Sasa
kibarua kinachofuata ni cha Antonio Conte kumuiga alichofanya Carlo
Ancelotti Mwaka 2010 alipotwaa Dabo katika Msimu wake wa kwanza na
Chelsea kwa hapo Mei 27 kwa kuifunga Arsenal Wembley katika Fainali ya
FA CUP.
Kwenye
Mechi nyingine ya EPL iliyochezwa Jana huko Goodison Park, Everton pia
iliitungua Watford 1-0 kwa Bao la Dakika ya 56 la Ross Barkley Mchezaji
ambae amegoma kusaini Mkataba Mpya akishinikiza kuhama.
0 Maoni:
Post a Comment