SIMBA wanaongoza VPL, Ligi Kuu Vodacom, baada ya jana kuifunga Stand United 2-1 kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Suleiman
Kassim ‘Selembe’ aliipa Stand United Bao kabla hata Dakika 1 kutimia
lakini JumaLuizio akaipigia Simba Bao 2 Dakika za 24 na 34 na kuipa
ushindi wa 2-1.
Ushindi huo wa jana umeiweka Simba kileleni mwa VPL wakiwa na Pointi 65 kwa Mechi 29 wakibakisha Mechi tu.
Lakini
uongozi huo wa Simba huenda ukafutwa leo Jumamosi ikiwa Mabingwa
Watetezi Yanga wataifunga Mbeya City kwenye Mechi itakayochezwa Uwanja
wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Yanga wapo Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 62 kwa Mechi 27 wakibakiza Mechi 3.
0 Maoni:
Post a Comment