Southampton, maarufu kama 'Watakatifu', imewafunga tena Liverpool 1-0 ndani ya Anfield katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England, na kutinga Fainali.
Kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali huko Saint Mary Southampton ilishinda 1-0 kwa Bao la Nathan Redmond na hivyo sasa kutinga Fainali kwa Jumla ya Bao 2-0.
Bao
la ushindi la Mechi ya Leo lilifungwa Dakika ya 92 na Shane Long
alietokea benchi baada ya kupokea pande zuri kwa kaunta ataki toka kwa
Sims ambae nae alitokea benchi.
Leo
Usiku, Mechi nyingine ya Marudiano ya Nusu fainali itachezwa huko KCOM
Stadium kati Ya Hull City na Manchester United ambao walishinda 2-0
katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Old Trafford.
Mshindi wa Mechi hii atacheza na Southampton ndani ya Wembley Jijini London hapo Februari 26.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Liverpool: Karius, Alexander-Arnold, Matip, Lovren, Milner, Can, Henderson, Lallana, Firmino, Sturridge, Coutinho.
Akiba: Wijnaldum, Klavan, Moreno, Lucas, Mignolet, Origi, Woodburn.
Southampton: Forster, Cedric, Stephens, Yoshida, Bertrand, Ward-Prowse, Romeu, Davis, Tadic, Rodriguez, Redmond.
Akiba: Clasie, Long, Martina, Hojbjerg, McQueen, Sims, Lewis.
Martin Atkinson |
0 Maoni:
Post a Comment