MECHI
za mwisho za Kundi D la AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika, zimekamilika Usiku huu huko Gabon na
kukamilisha safu ya Mechi za Robo Fainali baada ya Egypt kuilaza Ghana
1-0 na kufuzu na kuungana na hao Ghana waliofuzu kabla ya mechi hiyo.
Bao la ushindi ambalo limeiingiza Rgypt Robo Fainali limefungwa Dakika ya 11 na Mohamed Salah.
Katika
Mechi nyingine ya Kundi D, Uganda walitangulia kufunga Dakika ya 70 kwa
Bao la Farouk Miya na Mali kurudisha Dakika ya 73 kwa Frikiki ya Yves
Bissouma.
Robo Fainali zitaanza kuchezwa Jumamosi.
RATIBA YA ROBO FAINALI.
Jumamosi Januari 28
1900 Burkina Faso v Tunisia
2200 Senegal v Cameroon
Jumapili Januari 29
1900 Congo DR v Ghana
2200 Egypt v Morocco
Nusu Fainali
Jumatano Februari 1
2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4
Alhamisi Februari 2
2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3
Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2
Fainali.
Jumapili Februari 5
2200 Finalist 1 v Finalist 2
0 Maoni:
Post a Comment