VPL,
Ligi Kuu Vodacom, ipo kilingeni kuanzia Ijumaa kwa Mechi 1 na Jumamosi
ni lukuki yake lakini Siku hiyo ‘Macho Kodo’ yapo Jijini Dar es Salaam
kwa Bigi Mechi kati ya Simba na Azam FC na huko Sokoine, Mbeya kwenye
Dabi kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City.
Ijumaa
ipo Mechi moja huko CCM Kirumba Mwanza kati Ya Mbao FC na Ruvu Shooting
Timu ambazo zimepishana Pointi 4 wakati Ruvu Shooting ikiwa Nafasi ya 8
na ina Pointi 24 na Mbao FC wapo wa 12 wakiwa na Pointi 20.
Jumamosi zipo Mechi 4 na mbili kati ya hizo zina majina moja ikiwa ni BIGI MECHI na nyingine ni DABI.
BIGI
MECHI ipo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Simba na Azam FC
na DABI ni huko Sokoine Jijini Mbeya kati ya Tanzania Prisons na Mbeya
City.
Simba ndio Vinara wa VPL wakiwa mbele ya Azam FC, walio Nafasi ya 4, kwa Pointi 12.
Mbeya
City, ambao wako Nafasi ya 6, wamecheza Mechi 2 zaidi ya Tanzania
Prisons ambao wako Nafasi ya 9 wakiwa Pointi 4 nyuma yao.
Jumapili,
Mechi pekee ni Jijini Dar es Salaam ambayo huenda ikapigwa Uwanja wa
Taifa kama si Uhuru, ambapo Mabingwa Watetezi Yanga watakapokumbana na
Mwadui FC.
Yanga
wao wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba na Mwadui
FC wako Nafasi ya 10 wakiwa Pointi 21 nyuma ya Yanga.
***VPL – Ligi Kuu Vodacom Ratiba***
Ijumaa Januari 27
Mbao FC v Ruvu Shoooting
Jumamosi Januari 28
Toto Africans v African Lyon
Simba v Azam FC
Tanzania Prisons v Mbeya City
Ndanda FC v Majimaji FC
Jumapili Januari 29
Yanga v Mwadui FC
Jumatatu Januari 30
Kagera Sugar v Mtibwa Sugar
JKY Ruvu v Stand United
0 Maoni:
Post a Comment