LEJENDARI
wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametamka kuwa Rekodi ya Wayne
Rooney ya kuifungia Klabu hiyo Mabao 250 haitavunjwa.
Rooney,
mwenye Miaka 31, alifunga Bao lake la 250 kwa Klabu yake Manchester
United Jumamosi iliyopita katika Dakika ya 94 walipotoka 1-1 na Stoke
City huko Britannia Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Bao hilo lilivunja Rekodi ya Mfungaji Bora katika Historia ya Man United, Sir Bobby Charlton, aliyoishikilia kwa Miaka 44.
Mwaka Jana, Rooney pia aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton na kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Timu ya Taifa ya England.
Sir
Alex Ferguson, ambae alikuwa Meneja wa Man United tangu 1986 hadi 2013
na ambae pia ndie aliemchukua Roooney Mwaka 2004 kutoka Everton,
ameeleza: “Rekodi ilidumu Miaka 44 na wakati Rooney anajiunga
sikutegemea kama atavunja Rekodi ya Sir Bobby! Kufanya hilo ni kitu
kikubwa. Ni ajabu! Yeye amecheza kama Gemu 200 chini ya zile za Sir
Bobby. Na hilo ni ajabu zaidi!”
Aliongeza:
‘Sidhani kama kuna Mtu atampita Rooney. Siwezi kusema hapana, hapana
usiseme hapa, lakini ukitizama Soka la sasa, Man United ni moja ya Klabu
chache kabisa kuweka Mchezaji kwa Miaka 10!”
0 Maoni:
Post a Comment