Mshambuliaji Mbwana Samatta wa Genk kutupia mabao hii ikiwa ni mechi ya pili mfululizo.
Samatta amefunga wakati timu yake ikiitwanga Kortrijk kwa mabao 3-0 katika Ligi ya Ubelgiji.
Samatta amefunga bao la pili katika dakika ya 42 wakati Genk ikiwa inaongoza kwa bao moja.
Alejandro Pozuelo yeye alifunga bao katika dakika ya 68 kuhitimisha ushindi huo mnono wa Genk ikiwa nyumbani.
Mechi iliyopita Genk ikivaa Eupen, Samatta alifunga bao pekee na timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
0 Maoni:
Post a Comment