MECHI
za mwisho za Kundi C la AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika, zimekamilika Usiku wa kuamkia leo huko Gabon na
Mabingwa Watetezi Ivory Coast kutupwa nje baada kuchapwa 1-0 na Morocco
ambao wametinga Robo Fainali pamoja na Congo DR iliyoibandika Togo 3-1.
Mfungaji
Bora wa AFCON 2017, Junior Kabananga, ndie aliefunga Bao la kwanza kwa
Congo DR na wakafuata Mubele na M’Poku na Bao la Togo kuingizwa na Kodjo
Fo-Doh Laba.
Kwenye
Mechi ya Morocco na Ivory Coast, Bao la ushindi la Morocco lilifungwa
Dakika ya 64 na Rachid Alioui kwa kigongo cha Mita 25 na kumweka kidedea
Kocha wao Herve Renard ambae ndie aliiongoza Ivory Coast kutwaa Ubingwa
huu Mwaka 2015.
Jumatano
Usiku Mechi za mwisho za Kundi D ambazo ndizo za mwisho kabisa za
Makundi zitachezwa huku Ghana wakiwa tayari washafuzu Robo Fainali na
kuiacha ngoma iwe kwa Egypt na Mali nani kuungana nao wakati Uganda
wakiwa tayari wametupwa nje.
MSIMAMO:
0 Maoni:
Post a Comment