Mjadala wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele kuachia ngazi katika klabu hiyo umeshika kasi.
Mjadala
huo umekuwa na nafasi kubwa hasa mitandaoni, mashabiki wengi wa Simba
wakihoji sababu ya kuachia ngazi siku chache kabla ya kuivaa Azam FC
naye akiwa amerejea kuungana na Azam TV.
Kahemele
aliwahi kufanya kazi Azam FC, baadaye Azam TV kabla ya kujiunga na
Simba. Hii inaonyesha mashabiki hao wamekuwa na hofu kwa kuwa Simba
inakutana na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumamosi.
Jambo
hilo limesababisha mashabiki katika makundi mbalimbali hasa yale ya
Whatsapp na pia Facebook kuhoji, wengine wakidai huenda Kahemele alikuwa
mtego kwao.
Lakini
wako ambao wamekuwa wakiwatuliza wenzao na kuwataka kuwa na subira huku
wakiamini Kahemele ni mtu ambaye pia anatakiwa kuangalia maslahi ambayo
huenda yamemvuta.
Mara
ya mwisho zilipokutana, Simba ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC
katika fainali ya Kombe la Mapinduzi, hiyo inaweza ikawa hofu namba moja
ya Simba.
Lakini,
inaonekana Simba wana hofu kwa kuwa wana tofauti ya pointi mbili tu
dhidi ya Yanga, wao wana 45 na watani wao 43. Kama watapoteza na Yanga
ikaishinda Mwadui, Jumapili. Basi watapoteza uongozi wa ligi kuu.
0 Maoni:
Post a Comment